Jumatano, 9 Aprili 2014

Download K2 Ft. Doch Fleva - Huyu Demu | Hassbaby's (Mapacha)

 download hapa nyimbo mpya ya k2 kamshikisha doch fleva ngoma inaitwa huyu demu kutoka katika production ya Top music iliyopo mpwapwa Producer ni Sean J Javie

Download K2 Ft. Doch Fleva - Huyu Demu | Hassbaby's (Mapacha)

Jumamosi, 22 Machi 2014

RAIS WA MIDUARA BONGO LEO NDANI YA MPWAPWA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Zenji At anatarajiwa kkufanya bonge moja la shoo katika wilaya ya mpwapwa ndani ya ukumbi wa MANASSE INN hatari tupu  kama upoo mp usikose.

Jumatatu, 30 Desemba 2013

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASIMU YA PILI NA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Rasimu ya Katiba hii ni ndefu kuliko ya kwanza in ibara 271 ya kwanza ilikuwa na ibara 240 .Wananchi wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala bora  kama  ifuatavyo:



1-lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa.

2-Madaraka ya Rais yamepunguzwa.
3-wabunge wasiwe mawaziri
4-kuwe na ukomo wa wabunge
5-wananchi wawajibishe wabunge
6-spika/naibu wasiwe wabunge wala viongozi wa juu wa vyama vya siasa.

7-kuwepo na jeshi moja la Polisi na Usalama wa Taifa.

MUUNGANO
Muungano umependekezwa uwe wa serikali tatu kutokana  na  kero  mbalimbali  zilizoko pande zote mbili. Baadhi ya kero hizo ni kama ifuatavyo:

Kero za wazanzibar
1-Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Tanzania na hivyo kutumia mwanya huo kujipatia misaada toka nje
2-mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka
3-kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais

Kero za  Tanzania Bara.

1-Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamuhuri ya Muungano
2-Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar  wakati wazanzibar huku Tanganyika wanaruhusiwa


Mambo mengi ya Muungano yamebadilishwa bila kufuata Katiba. HIVYO:
 

** TUME imependekeza  muundo wa muungano uwe  wa  serikali 3.

Jumatano, 27 Novemba 2013

ICC YATAKA KENYATTA KUWEPO MAHAKAMANI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Mahakama ya Kimataifa ya kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita, ICC imetengua uamuzi wake wa awali uliomruhusu Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili.
Mahakama hiyo sasa imesema kuwa ni lazima Bwana Kenyatta afike binafsi mbele ya mahakama hiyo kusikiliza kesi yake na ushahidi unaotolewa dhidi yake.
Mahakama hiyo imesema kama sheria inavyotaka, Bwana Kenyatta lazima binafsi ahudhurie vikao vya kesi inayomkabili. Imesema maombi yoyote ya baadaye ya kutaka asihudhurie baadhi ya vikao vya kesi hiyo, yatafikiriwa kutokana na msingi wa suala linaloombewa ruhusa hiyo.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi kwamba hukumu iliyotolewa katika rufaa ya tarehe 25 Oktoba 2013 ya Mwendesha mashitaka dhidi ya William Samoei Ruto na Joshua Arap Sang, imetoa taarifa mpya muhimu ambayo inahalalisha kuangaliwa upya kwa suala la kesi hiyo.
Fatou Bensouda,Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC
Mahakama ya Rufaa ya ICC imehitimisha kuwa Mahakama ina hiyari kwa mujibu wa kifungu namba 63(1), kinachosema kuwa "mtuhumiwa ni lazima awepo mahakamani wakati kesi inayomkabili ikiendeshwa", lakini hiyari hiyo imewekewa kikomo. Mahakama ya Rufaa imetoa uamuzi kwamba mtuhumiwa kutofika mahakamani, inaruhusiwa pale tu panapokuwa na sababu maalum na za kipekee, na lazima sababu hizo ziwe zinakidhi hoja kwa mtuhumiwa kutofika mahakamani hapo.Imeendelea kusema kwamba uamuzi wa kama mtuhumiwa aruhusiwe kutohudhuria sehemu ya vikao vya kesi yake lazima uzingatie hali halisi ya ombi la mtuhumiwa.
Awali mahakama hiyo ya ICC katika uamuzi wake wa tarehe18 October 2013, ilitoa masharti kwa upande wa utetezi wa Bwana Uhuru Muigai Kenyatta kuwepo mahakamani hapo wakati wa ufunguzi na kufunga kesi inayomkabili badala ya kuwepo wakati wote. Wakati huo angeweza kusikiliza maelezo kutoka pande zote na kusikiliza maoni ya waathirika wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 nchini Kenya. Pia angetakiwa kuwepo siku ya kufunga kesi hiyo kwa kusikiliza hukumu yake.
Kutokana na uamuzi huo wa kumruhusu Bwana Kenyatta kuhudhuria vikao vya ufunguzi na kufunga kesi yake pamoja na vikao vingine ambavyo angeitwa pale mahakama inapoona umuhimu wa yeye kuwepo mahakamani, mwendesha mashitaka alipinga uamuzi huo tarehe 28 Oktoba 2013, kwa kukata rufaa, akitaka kuangaliwa upya kwa uamuzi wa tarehe 18 Oktoba 2013, ambapo mwendesha mashitaka aliomba mahakama kufuta uamuzi wake wa kumruhusu mtuhumiwa kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi yake na badala yake mahakama izingatie sheria kuu chini ya kifungu cha 63(1).
Bwana Kenyatta ameshitakiwa kama mchochezi asiye rasmi, akikabiliwa na mashitaka matano ya uhalifu dhidi ya binadamu, yakiwemo mauaji, kuhamishwa watu kwa nguvu, ubakaji, utesaji na vitendo vingine visivyo vya kibinadamu, vinavyodaiwa kufanyika wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007-2008.
Mashitaka dhidi yake yalithibitishwa tarehe 23 Januari 2012, na kesi hiyo kukabidhiwa Chemba namba V(b) ya mahakama hiyo ya ICC. Kesi yake imepangwa kuanza kusikilizwa katika mahakama hiyo tarehe 5 Februari 2014.

MIRAA HAIZIDISHI UGAIDI "FLORENCE KAJUJU"

Akiwaongoza wabunge wenzake katika kulishawishi bunge la Uingereza kutopitisha sheria za kupiga marufuku miraa kutoka Kenya kuingia nchini Uingereza, mbunge Florence Kajuju, kutoka jimbo la Meru nchini Kenya, ameielezea BBC akiwa London kwamba uchunguzi wao unaonyesha mapato ya biashara ya miraa kamwe hayana uhusiano na ugaidi.
Ameelezea kwamba utafiti wao umegundua kwamba kuna kampuni mbili tu ambazo huingiza miraa nchini Uingereza, na hakuna ushahidi wowote kuonyesha mapato yao hutumiwa katika kuendeleza ugaidi.
Kuhusiana na madai ya athari za afya, anasema wamezungumza na wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, na ambao wamesema miraa haina hatari zozote za kiafya.
Anasema miraa haiwezi kufikiriwa kama mihadarati.
"Ile kitu imetufurahisha zaidi ni kwamba ripoti iliyofikishwa katika bunge la Uingereza kutoka kwa kamati inayotoa ushauri kuhusiana na utumizi usiofaa wa dawa ilisema ya kwamba miraa sio dawa ya kulevya na kwa hiyo haikuielezea serikali ya Uingereza ipige marufuku miraa", alielezea.
Mbunge Kajuju anasema kwa kiasi fulani, ujumbe wao umeanza kuwashawishi baadhi ya wabunge wa Uingereza na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa zao la miraa, na kwamba haina athari zozote za kiafya.
Lakini anaelezea kazi yao sio rahisi, kwani "huyu mama ambaye ni waziri wa masuala ya nyumbani wa Uingereza ameendeleza, na amefikisha muswada bungeni akiomba sheria ipitishwe ya kupiga marufuku miraaa na ndio sababu tuliona ni afadhali tuje na tuzungumze na wabunge wenzetu tuwaelezee na kuleta ripoti tuliyoileta kutoka Kenya kutoka kwa wanasayansi wetu wa Kenya kuwaonyesha kwamba miraa haina shida yoyote".
Zao la miraa linategemewa sana kiuchumi na wakulima wengi katika maeneo ya Meru na Embu nchini Kenya.

Jumatatu, 25 Novemba 2013

WASHIRIKA WA BAMBE WAFIKISHWA MAHAKAMANI ICC

Washirika wanne wa aliyekuwa naibu rais wa DRC, Jean-Pierre Bemba, wamekamatwa kwa madai ya kuhitilafiana na ushahidi dhidi ya Bemba katika kesi inayomkabili katika mahakama ya ICC.
Mahakama hiyo imethibitisha kuwa washukiwa wanne waliokamatwa ni pamoja na mawakili wa Bemba, pamoja na aliyekuwa karani wake.
Kesi dhidi ya kiongzoi huyo wa zamani wa waasi, imekuwa ikiendelea tangu Novemba mwaka 2010, ambapo anatuhumiwa kwa makosa ya mauaji , ubakaji na uporaji katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
Mahakama ya ICC katika taarifa yake imesema kuwa washukiwa hao pia waliwasilisha stakabadhi bandia kwa mahakama hiyo.
Jean Pierre Bemba ni kiongozi wa upinzani pamoja na kuwa kiongozi wa waasi ambaye alifikishwa Hague kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
ICC imetoa vibali vya kukamatwa kwa watu 5 akiwemo Bemba, lakini pia, mawakili wake wawili, shahidi mmoja na mbunge kutoka kwa chama chake walikamatwa.
Wanatuhumiwa kuwa sehemu ya mtandao wa watu waliowasilisha stakabadhi bandia kwa mahakama ya ICC pamoja na kuwapa mlungula baadhi ya mashahidi ili watoe ushahidi wa uongo katika kesi dhidi ya Bemba.
Jean Pierre Bemba amezuiliwa Hague tangu mwaka 2008 kwa makosa anayodaiwa kuyafanya katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati,kati ya mwaka 2002-2003. Washirika wake walikamatwa na polisi nchini DRC, Ufarnsa , Ubelgiji na Uholanzi.
Mahakama inasema kuwa watapelekwa Hague jkatika muda mfuypi ujao.
Afisaa mmoja wa ICC aliambia BBC kuwa ikiwa watapatikana na hatia huenda watkatumia kifungo cha miaka mitano gerezani

Jumamosi, 23 Novemba 2013

10 KIZIMBANI KWA MAUAJI YA DK. MVUNGI

Hatimaye
watu Kumi wanaodaiwa kumuua Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Sengondo Mvungi Jana walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam, wakikabiliwa na kosa Moja tu la kumuua Dk.Mvungi kwa kukusudia. Wakili wa serikali Aida Lusumo Mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni chibago Magoze (32),John Kanjunju(29),John Mayunja,Longishu Losingo(29),''Masunga Makunza,Paulo Dondondo(30),mkanda Mlewa(40),zakaria msese(33),msungwa Matonya(30) na Ahmed kilebu(30). Wakili Lusumo alidai wanashitakiwa kwa kosa la Kua kwa kukusudia kinyume na kifungo Cha 196 Cha Sheria ya kanuni a adhabu ya Mwaka 2002 , Kuwa Novemba 11 Mwaka 2013 huko eneo la msakuzi kino done Dar es salaam, wote kwa pamoja walimuua Dk.Mvungi ambaye alikuwa ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es salaam na kwamba upelelezi bado haujakamilika. Hakimu Fimbo aliwataka washitakiwa Hao wasiyonaidai chochote kwasababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza Kesi hiyo hivyo akaamuru washitakiwa wapelekwe gerezani. Washitakiwa walifikishwa chini ya Ulinzi MKALI wa wanausalama AMBAPO walipandishwa Kwenye Gari aina ya Landcruser yenye namba za usajili KX 06EFD na walisikikiza na Gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 539 CCB ambalo Lilikuwa likiongoza msafara huo. Chanzo:Tanzania Daima la Jumamosi ,Novemba 23 Mwaka 2013

TAARIFA KWA WATANZANIA JUU YA UAMUZI WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU KUWAVUA NYADHIFA ZA UONGOZI NAIBU KATIBU MKUU, MH. ZITTO ZUBERI KABWE NA WENZAKE

Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,

         Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya siku ya Jumatano ya tarehe 20 Novemba, 2013 hadi alfajiri ya leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2013 imetafakari na kujadili kwa kina taarifa mbali mbali juu ya hali ya kisiasa ndani na nje ya Chama chetu ambayo kwa muda mrefu imegubikwa na tuhuma kubwa na nzito dhidi ya Chama chetu na viongozi wake wakuu, yaani Mwenyekiti wa Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (MB), na Katibu Mkuu, Dk. Wilbrod Peter Slaa. Tuhuma hizi zilikuwa na malengo na athari ya kuwapaka matope na kuwachafua viongozi wakuu wa Chama na Chama chenyewe, kutengeneza mtandao wa siri ndani na nje ya Chama ambao hatimaye ungefanikisha sio tu lengo la kufanya mapinduzi nje ya utaratibu wa kikatiba wa Chama, bali pia ungekipasua Chama vipande vipande na hivyo kuua matumaini ya Watanzania juu ya uwezekano wa kufanya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na kijamii katika nchi yetu kwa kukiondoa madarakani Chama cha Mapinduzi (CCM).

          Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Uchunguzi wa Kamati Kuu umebaini kuwepo kwa mkakati mkubwa wa kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013.’ Mkakati huu uliandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’ ambacho vinara wake wakuu ni wanne, yaani Naibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambaye kwenye waraka huo anajulikana pia kama ‘MM’ au ‘Mhusika Mkuu’; mjumbe wa Kamati Kuu na mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitilla Mkumbo ambaye kwenye waraka anajulikana pia kama M1; Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa amesimamishwa uongozi, Bwana Samson Mwigamba na ambaye kwenye waraka anaitwa M3; na mtu mwingine ambaye hadi sasa jina lake halijajulikana lakini kwenye waraka anajulikana kama M2 na anatajwa kuwa yuko ‘ukingoni kupigwa nje’ katika mageuzi ya kiutendaji yanayoendelea katika Sekretariat ya Chama hapa Makao Makuu.

       Kwa mujibu wa waraka wenyewe, “Mkakati huu umeandaliwa kwa pamoja na M2 na M3 na kupitiwa na kurekebishwa na M1 ili upelekwe kwa MM kwa maoni ya mwisho na kuanza utekelezaji.” Mbele ya Kamati Kuu, Dk. Mkumbo alikiri kwamba MM au Mhusika Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe; M1 ni yeye mwenyewe Dk. Mkumbo na M3 ni Bwana Mwigamba. Dk. Mkumbo alikataa kata kata kumfahamu M2. Aidha, Dk. Mkumbo alikiri mbele ya Kamati Kuu kwamba yote yaliyoandikwa katika ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ yametoka kwenye ‘Mtandao wa Ushindi’ na hayajabadilishwa.

          Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango wa kuipasua pasua CHADEMA na kuiangamiza kabisa kwenye uso wa siasa za Tanzania. Huu sio mkakati wa kufanya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya Chama kwa njia za kidemokrasia na za kikatiba. Ni mpango wa kukiteka nyara Chama na kukiua. Ndio maana watunzi wa waraka huu wamesema kwenye waraka wao: “Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu aliyepo aendelee kubweteka na ndio maana hata lugha iliyotumika ndani hapa ni ya pekee.” Kamati Kuu inaamini mkakati wenye malengo halali ya kufanya mabadiliko ndani ya Chama kwa njia halali za kikatiba usingependekeza kwamba: “Vikao vyetu na yeye (MM aka Mhusika Mkuu aka Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe) vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.” Aidha, Kamati Kuu inaamini kwamba kama mkakati huu ungekuwa na malengo mazuri ya kukijenga Chama na sio kukiteka nyara na kukiua, wanamtandao hawa wasingependekeza utaratibu ufuatao wa utekelezaji wa mpango: “M1 (Dk. Mkumbo) ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms. M1 ndiye atakayewasilisha mambo yote yanayotoka kwenye kamati ya kitaifa na endapo kuna haja ya MM kukutana na kamati ya kitaifa, mipango yote ya kikao itafanywa na M1 kwa usiri mkubwa.”

        Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango haramu na ambao unaichana chana Katiba ya Chama chetu. Ni mkakati wa vita dhidi ya Chama chetu na utaratibu wetu wa kikatiba. Wakati ibara ya 10.1(iv) ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama ambazo ni sehemu ya Katiba ya Chama chetu ya mwaka 2006 inamkataza kiongozi wa CHADEMA asijihusishe na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini, au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya Chama na miongoni mwa jamii kisiasa au kijamii”, wanaMtandao wa Ushindi wameonyesha wazi kuwa wanaendekeza siasa za udini kwa kusema yafuatayo juu ya waliemwita ‘mtu tunayemtaka’, yaani Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe: “Kwa kuwa ni Mwislamu, hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.”

            Wakati ibara ya 10.1(viii) ya Kanuni za Uendeshaji inamtaka kila kiongozi wa CHADEMA “... kuwa mkweli na muwazi wakati wote ... na aachane na vikundi vya majungu na wadanganyifu (rumour mongers) ...”, wanaMtandao wa Ushindi wameeleza kwenye waraka wao kwamba mipango yao ya utekelezaji wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 ‘itafanyika kwa usiri mkubwa.’ Wakati ibara ya 10.1(ix) ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama inamtaka “kiongozi asijihusishe na vikundi na vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama wake”, wanaMtandao wa Ushindi wamesambaza tuhuma za uongo dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa (ambaye wanamwita kwenye waraka wao kuwa ni ‘Mpinzani wetu’) kuwa “... hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii.... Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi za chini hivi sasa na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka.”

            Wakati ibara ya 10.1(x) ya Kanuni za Uendeshaji inamtaka “kiongozi asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Kanuni”, tuhuma zote zilizotolewa na wanaMtandao hawa dhidi ya viongozi wakuu wa Chama chetu hazijawahi kutolewa na yeyote kati ya wanaMtandao hawa katika kikao chochote halali cha Chama cha ngazi yoyote.

         Wakati ibara ya 10.1(xii) ya Kanuni za Uendeshaji inaeleza kwamba “itakuwa marufuku kwa kiongozi wa CHADEMA kukashifu Chama, kiongozi au mwanachama yeyote wa Chama ...”, Mkakati wa Mabadiliko 2013 umejaa kashfa kubwa, matusi mengi na udhalilishaji mkubwa wa Chama, viongozi wake wakuu na wanachama kwa ujumla. Hivyo, kwa mfano, Mwenyekiti wa Chama Taifa ametuhumiwa na wanaMtandao hawa kuwa ni mtu mwenye ‘uzalendo unaotia shaka’, mwenye ‘elimu ya magumashi’, ‘mzito kujieleza’, ‘mtu mwenye akili ndogo’, n.k.

          Ndugu wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Hakuna chama au taasisi yoyote duniani inayoweza kunyamazia mkakati wa aina hii dhidi yake na viongozi wake wakuu na ikadumu au kubaki salama. Chama au taasisi yoyote inayoendekeza vitendo vya aina hii miongoni mwa viongozi wake wa ngazi yoyote au miongoni mwa wanachama wake wa kawaida inakaribisha kifo na mauti. Chama chetu na viongozi wake wa juu wamekaa kimya kwa muda mrefu sana; wamevumilia mashambulizi na kashfa nyingi sana dhidi yao binafsi na dhidi ya Chama; wamestahimili matusi makubwa sana dhidi yao. Chama chetu kimevumilia yote haya na viongozi wake wamevumilia yote haya sio kwa sababu walitaka Chama chetu kiuwawe na wanaMtandao hawa. Uvumilivu wote huu ulitokana na haja ya kuwapa wanaMtandao wa Ushindi fursa ya kugundua hatari ya siasa zao na kuwapa muda wa kujirekebisha na kujirudi.

          Kama ilivyo kwa binadamu au taasisi yoyote ile, uvumilivu wa Chama chetu na viongozi wake wakuu una kikomo. Na hiki ndio kikomo cha uvumilivu wa Chama chetu, viongozi wake na wanachama wake kama wanavyowakilishwa na Kamati Kuu ya Chama chetu. Hivyo basi, katika kikao chake tajwa, Kamati Kuu ya Chama chetu, kwa kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya dharura chini ya ibara ya 6.5.2(d) ya Katiba ya Chama, imeazimia yafuatayo kuhusu Mkakati wa Mabadiliko 2013 na hao wanaojiita wanaMtandao wa Ushindi:

       Kwamba, kuanzia sasa, viongozi wote waliohusika ama kuhusishwa na mkakati huu, yaani Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mjumbe wa Kamati Kuu Dk. Kitilla Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba wavuliwe nyadhifa zao zote za uongozi ndani ya Chama; Kwamba timu ndogo ya pamoja ya watendaji wa Sekretariat ya Makao Makuu ya Chama na wajumbe wa Kamati Kuu ifanye uchunguzi wa haraka ili kumtambua mtu anayeitwa M2 na ambaye anadaiwa kuwa mtumishi wa Makao Makuu ya Chama ili hatua stahiki na za haraka zichukuliwe dhidi yake, pamoja na watu wengine wote watakaobainika kuhusika na mpango huu wa uhaini dhidi ya Chama chetu; Kwamba Kamati ya Chama ya Wabunge inaelekezwa kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe anavuliwa madaraka yake yote kama Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, with immediate effect;

      Kwamba viongozi waliotajwa katika aya ya (a) waandikiwe hati zenye tuhuma dhidi yao haraka iwezekanavyo na watakiwe kujieleza kwa nini wasifukuzwe kwenye Chama kwa vitendo vyao na wapatiwe fursa kamili ya kujitetea kama inavyotakiwa na ibara ya 6.5.2(a), (b) na (c) ya Katiba ya Chama; Kwamba mara baada ya utekelezaji wa azimio (d), Kamati Kuu ikutane kwa dharura kwa ajili ya kufanya uamuzi juu ya hatma ya watuhumiwa na hatua nyingine zitakazofuata; Kwamba waraka wa wanaojiita wanaMtandao wa Ushindi uwekwe hadharani na usambazwe kwa vyombo vya habari vya aina zote ili wananchi wa Tanzania, wanachama na viongozi wa Chama chetu na dunia nzima kwa ujumla iweze kupima uzito wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 na uhalali wa maamuzi haya ya Kamati Kuu.

          Ndugu wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu Dk. Kitilla Mkumbo waliiomba Kamati Kuu iwaruhusu kujiuzulu nyadhifa zao baada ya Mkakati wao wa kukiteka nyara Chama na kukiangamiza kujulikana mbele ya Kamati Kuu. Kwa kuzingatia uzito wa makosa waliyokifanyia Chama, viongozi wake wakuu na wanachama wake kwa ujumla; na kwa kuzingatia uzito na umuhimu wa nyadhifa kubwa walizo nazo ndani ya Chama; na kwa kuzingatia uelewa wao wa Katiba, Kanuni na taratibu za Chama na uzoefu wao katika safu za juu za uongozi wa Chama, Kamati Kuu ilikataa kwa kauli moja kuridhia maombi hayo ya kujiuzulu. Kufanya hivyo ingekuwa ni sawa na kuwaruhusu wajiondoe kwenye uongozi wa Chama wakiwa na heshima wasizostahili hata kidogo.

         Chama chetu ni tumaini pekee la Watanzania wote wanaotaka mabadiliko ya kweli na ya kimsingi katika mfumo wa kiutawala, kiuchumi na kijamii wa nchi yetu. Hii ndiyo sababu kubwa na ya pekee iliyosababisha vita kubwa na chafu inayopigwa dhidi ya Chama chetu na viongozi wetu wakuu. Lengo kuu ni kuwachafua viongozi wakuu, kuleta mgogoro na mgawanyiko ndani ya wanachama, viongozi wake na hivyo kukichafua Chama mbele ya macho ya Watanzania. Chama chetu kikishachafuka kwa mtindo huu, matumaini ya Watanzania wanaotaka mabadiliko yatakufa. Vita hii kubwa haijaanza jana, na haitaisha kesho. Kama ambavyo tumekabiliana nayo na kuishinda siku za nyuma, vivyo hivyo tutakabiliana nayo mara hii na kuishinda. Kama Chama chetu kilivyoibuka na nguvu na heshima kubwa zaidi katika mapambano ya siku za nyuma, vivyo hivyo Chama chetu kitaibuka na nguvu na heshima kubwa zaidi katika awamu hii ya mapambano.

         Tunawaomba Watanzania, wanachama na viongozi wetu wasife moyo, bali waendelee kukiunga mkono chama chao cha ukombozi. Tunawaomba Watanzania, wanachama na viongozi wetu waendelee kulilinda tumaini lao pekee la mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi yetu. Badala ya kukatishwa tama, kila mmoja wetu aongeze bidii maradufu ili kuwashinda wale wanaotaka kuleta majanga katika Chama chetu na kwa Taifa letu.

------------------------------------------
FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) - MWENYEKITI, TAIFA

------------------------------------------
WILBROD PETER SLAA - KATIBU MKUU

Jumamosi, 16 Novemba 2013

WATU WATANO WAKAMATWA NA PEMBE ZA TEMBO ZANZIBAR

Polisi nchini Tanzania wamesema shehena ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar ni sawa na Tembo mia tatu na watano, zikiwa na thamani ya karibu shilingi bilioni nane, sawa na karibu dola milioni tano za Kimarekani.
c55 Watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na pembe hizo, huku maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, na mmoja wa Mamlaka ya Bandari pia wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Kwa mujibu wa afisa habari mkuu wa jeshi la polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, watuhumiwa wa kesi hii watafikishwa katika mahakama jijini Dar es Salaam.
Pembe hizo zilikuwa zimefichwa kwenye kontena la urefu wa mita 40, tayari kwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Serikali ya Tanzania iko katika kampeni kamambe ya kupambana na ujangili ili kunusuru wanyama pori ambao wako hatari kutoweka kutoka na kushamiri kwa biashara ya meno ya tembo na vipusa vya faru.
Iliripotiwa kuwa wastani wa tembo 30 huuawa kila siku nchini Tanzania, hali iliyoilazimisha serikali kukabiliana na mtandao wa ujangili, ambao unatuhumiwa kuunganisha watu wa kada mbalimbali, wakiwemo wawindaji, wasafirishaji na wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya nchi.
Hivi karibuni raia watatu wa China walikamatwa nchini Tanzania kwa kukutwa na pembe 706 ya tembo, sawa na Tembo 353 waliouawa katika hifadhi mbalimbali nchini humo.

U.N YAKATAA KUAHIRISHA KESI YA KENYA

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, limekatalia mbali ombi la kuahirishwa kwa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.
Azimio hilo lililokuwa limependekezwa liliungwa mkono na nchi wanachama wa Muungano wa Afrika.
Viongozi hao wawili wanatuhumiwa kwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-08 nchini Kenya.
Kukataliwa kwa azimio hili ni changamoto ya hivi punde kwa kesi inayowakabili Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto wanaotuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-08.
Lakini azimio hilo lilipata tu kura saba badala ya angalau tisa ambazo zilihitajika kupitishwa na baraza la usalama la UN.
Nchi nane wanachama wa baraza la usalama la UN, nchi wanachama wote wa ICC, Uingereza, Ufaransa na Marekani zote zilijizuia kupiga kura kuhakikisha kuwa azimio hilo halipiti.
Ilikuwa mara ya kwanza katika miaka kumi kwa baraza la usalama la UN kukosa kupigia kura azimio kama hilo bila ya kutumiwa kwa kura ya turufu na mwanachama wa kudumu wa UN.
Mataifa ya Afrika yakiongozwa na Rwanda, iliyopendekeza azimio hilo, yalikosolewa vikali kwa kupendekeza azimio hilo na kulazimisha baraza la Usalama la UN kupiga kura.
Balozi wa Guatemala katika Umoja wa Mataifa, alisema kuwa jaribio la kutaka kuahirisha kesi hiyo ilikuwa njama ya hujuma dhidi ya nchi zinazotaka kusaidia Afrika na juhudi za amani pamoja na kuimarisha uwajibikaji wa viongozi katika mataifa hayo.
Kenyatta na Ruto wanatuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi Kenya, mwaka 2007 ambapo takriban watu 1,100 walifariki.
Kenyatta na Ruto walichukua hatamu za uongozi baada ya uchaguzi uliofuata mwaka 2013

Jumapili, 10 Novemba 2013

RAIA WA KIGENI ANASWA NA MAFUVU BURUNDI

Polisi nchini Burundi wanasema zaidi ya mafuvu 40 ya binadam yamepatikana katika makao ya raia mmoja wa Italia anayefanya kazi nchini humo.
Giussepe Favaro alikamatwa mwezi uliopita baada ya mafuvu mawili yaliyonuiwa kusafirishwa kwa ndege kunaswa katika uwanja wa ndege nchini Burundi.
Kwa mujibu wa polisi mafuvu hayo yalinuiwa kusafirishwa hadi nchini Thailand.
Polisi hata hivyo hawajatoa taarifa zaidi na mwandishi wa BBC nchini Burundi anasema watu wana shauku ya kutaka kujua mafuvu hayo yalitoka wapi na yalikua yatumike kivipi.
Kumekuwepo ripoti za sehemu za miili ya binadam kutumika katika ushirikina hasa katika nchi jirani ya Tanzania,lakini haifahamiki kwanini mafuvu yaliyopatikana hapo awali yalikua yakipelekwa Thailand.
Bw Favaro amekua akiishi nchini Burundi kwa miaka kadhaa.

MWENDESHA MASHTAKA AUAWA LIBYA

Mwendesha Mashtaka Mohammed al Naass ameuawa kwa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika mji wa bandari wa Darna mashariki mwa Libya.
Wakati huo huo polisi wawili wamepigwa risasi katika mji wa Benghazi ambapo ni wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch linasema karibu watu hamsini wameuawa tangu mwaka 2012 katika matukio yanayohusiana na mgogoro wa kisisiasa katika miji miwili iliyopo mashariki.
Pia kumekuwa na hali machafuko katika mji kuu wa Tripoli tangu mwishoni mwa wiki wakati makundi mawili ya wapiganaji yalipopambana kwa kutumia bunduki na silaha nzito nzito na kufanya milio ya makombora kusikika katika baadhi ya maeneo ya mji huo.
Karibu watu kumi wameripotiwa kujeruhiwa katika ghasia hizo.

Alhamisi, 7 Novemba 2013

KAMANDA WA M23 AJISALIMISHA UGANDA

Maafisa wa Serikali ya Uganda wanasema kuwa kamanda wa kijeshi wa wapiganaji walioshindwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, M23, amejisalimisha kwa utawala wa Uganda.
Ripoti kutoka Uganda zinasema kuwa mamia ya
wapiganaji wamejisalimisha pamoja na kiongozi wao, Sultani Makenga.
Wapiganaji hao wamejisalimisha katika eneo la hifadhi ya Wanyama ya Pori ya Mgahinga, kwenye mpaka wa Uganda na DRC.
Mnamo Jumanne M23 walisema kuwa wamesitisha maasi yao ya miezi 20 Mashariki mwa Congo, baada ya kutimuliwa katika ngome zao Mashariki mwa Congo na wanajeshi wa Serikali wakishirikiana na askari wa kudumisha amani wa Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo serikali za Uganda na DRC hazijaweza kuthibitsha madai haya.
Mapema wiki hii, M23 ilisema kuwa inamaliza uasi wake wa miezi kumi na tisa masaa chache baada ya majeshi ya serikali kudai ushindi dhidi ya waasi hao.
Ripoti zinasema kuwa Sultani Makenga na waasi wengine 1,700, wamesalimisha silaha zao na wanazuiliwa na jeshi la Uganda katika kambi ya jeshi ya Mgahinga, karibu na mpaka na DRC.
Mapema wiki hii, maafisa wa DRC walisema Makenga alitoroka na kuingia Uganda au Rwanda.
Uganda imekuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya waasi na serikali ya DRC , ingawa hakuna mkataba wa amani umefikiwa.

Jumatano, 6 Novemba 2013

PIKI PIKI MARUFUKU KUINGIA MONROVIA

Mamia ya wakaazi wa mji mkuu wa Liberia Monrovia, wamelazimika kwenda kazini kwa miguu baada ya sheria inayoharamisha bodaboda kuingia mjini humo kuanza kutumika.
Polisi waliweka vizuizi barabarani hasa katika maeneo muhimu ya kuingia mjini kuhakikisha huwa madereva wa pikipiki wanatii sheria hiyo.
Hatua ya serikali inatokana na tuhuma dhidi ya madereva wa pikipiki hizo ambazo hutumiwa kwa uduma za Taxi, kwa kuziendesha ovyo na kusababisha ajali nyingi barabarani.
Pikipiki hizi ambazo humilikiwa na watu binafsi, hutumiwa sana na wasafiri wengi mjini Monrovia na pia katika miji mingi barani Afrika.
Baadhi ya madereva wa pikipiki hizo huwabeba hadi watu watano wakati wanaruhusiwa tu kuwabeba watu wawili.
Kwa mujibu wa taarifa ya poliisi, madereva wowote wa pikipiki hizo watakaopatikana mjini watatozwa faini ya dola miambili.
Mmoja wa madereva hao Daniel Howard alisema kuwa wameghadhabishwa mno na hatua ya serikali.
Mwandishi wa BBC mjini Monrovia, Jonathan Paye-Layleh anasema kuwa sio mara ya kwanza kwa maafisa wa serikali kujaribu kuzuia pikipiki hizo kuingia katikati mwa mji.
Mapema mwaka huu madereva wa Pikipiki hizo walizuiwa kuziendesha katika baadhi ya barabara za mji baada ya saa nne usiku.
Hata hivyo sheria hii ya sasa inasemekana kutatiza usafiri pakubwa mjini humo.

KIPIGO CHAPELEKEA M23 KUACHA UASI

Waasi wa M23 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametangaza kumaliza uasi wao ndani ya nchi hiyo muda mfupi baada ya kupigwa katika ngome yao ya mwisho na majeshi ya serikali ya Congo yakishirikiana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupigana na waasi hao.
Katika taarifa walioitoa waasi hao wamesema badala ya kufanya uasi sasa wataendesha harakati zao kutumia njia ya kisiasa.
Muda mfupi uliopita Kiongozi wa waasi hao Bertrand Bisimwa ametangaza kuwaamuru mkuu wa wapiganaji wa M23 na makamanda wa vikosi vyote muhimu wa kundi hilo kuwaandaa wapiganaji wao kusalimisha silaha, kutawanyika kuondoka katika eneo la mapigano na kukubaliana na matakwa yatakayowekwa na serikali ya Congo
Awali Msemaji wa Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Lambert Mende aliambia BBC kuwa majeshi ya nchi yameishambulia ngome ya mwisho ya waasi na wamekimbia na wengine huenda wakawa wamejisalimisha.
Majeshi ya serikali ya Kongo yakishirikana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi hao walianza mapambano dhidi ya M23 Octoba mwaka huu na kufanikiwa kuwaondoa katika eneo la Bunagana kwenye mpaka wa Uganda ambayo ni ngome yao muhimu.

MILIPUKO NJE YA OFISI ZA CHAMA TAWALA NCHINI CHINA

Msururu wa milipuko midogo nje ya afisi za kimkoa za chama tawala cha Kikomunisti,imesababisha kifo cha mtu mmoja
Maafisa wa polisi katika eneo hilo wamesema kuwa milipuko hiyo ilisababishwa na mabomu madogo yaliyotengenewa nyumbani.
Mlipuko huo uliotokea muda wa asubuhi wenye shughuli nyingi, ulisababisha kuvunjika kwa madirisha na moshi mkubwa kufuka.
Ripoti zilizotolewa na shirika la habari la kiserikali zilisema kuwa mabomu madogo yalikuwa yamefichwa ndani ya maua kando ya barabara.
Milipuko hiyo ilitokea Kaskazini mwa China katika eneo la, Tai-yuan, mkoani, Shanxi,
Taarifa za vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa watu 8 wamejeruhiwa na magari mawili kuharibiwa.
Picha zilizowekwa kwa mitandao ya kijamii imeonyesha moshi ukifuka pamoja na magari ya wazima moto ikiwa katika eneo la shambulizi ambalo lilitokea mapema asubuhi ya leo.
Hakuna taarifa za kina kueleza kiini cha milipuko hiyo. Hata hivyo kumekuwa ma matukio ya mara kwa mara ya wananchi kufanya mashambulizi kama haya dhidi ya serikali hasa wale ambao hawahisi kuridhishwa na serikali hiyo.
Hali ya wasiwasi pia imetanda hasa baada ya tukio la wiki jana mjini Beijing ambalo mamafisa walisema kuwa lilikuwa njama ya shambulizi la kigaidi.

Jumatatu, 4 Novemba 2013

WASHUKIWA WANNE WA SHAMBULIO LA WEST GATE MAHAKAMANI

Wanaume wanne wamefikishwa mahakamani nchini Kenya baada ya kuhusishwa na shambulizi la kigaidi lililofanyika dhidi ya jengo la Westgate nchini Kenya mwezi Septemba.
Wanne hao wote walikanusha mashitaka hayo ikiwemo kosa la kuingia nchini bila vibali halali pamoja na kumiliki stakabadhi bandia za kujitambulisha.
Mahakama imeamuru wawekwe rumande.
Kundi la kigaidi la Somalia, Al Shabaab lilikiri kufanya shambulizi hilo la kigaidi ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.
Wanne hao walishitakiwa kwa kosa la kuhusika na shambulizi hilo la kigaidi ingawa hakuna hata mmoja alikuwemo ndani ya Jengo la Westgate wakati wa shambulizi hilo.
Wanne hao raia wa Somalia ni Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah, Adan Adan na Hussein Hassan.
Washukiwa hao ambao hawakuwa na mawakili walizuiliwa rumande kwa wiki moja baada ya kiongozi wa mashitaka kuomba muda zaidi kufanya uchunguzi.

MOHAMMED MORIS MAHAKAMANI MISRI

Kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi imeanza ambapo kiongozi huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi wa mauaji ya waandamanaji.
Kesi hiyo inafanyika katika kituo cha mafunzo ya polisi ambapo kuna ulinzi mkali
Wanachama wengine 14 wa ngazi za juu wa kundi la Muslim Brotherhood pia wameshitakiwa na mashatka kama hayo.
Vyombo vya habari vya kitaifa vimeripoti kwamba jaji wa kesi hiyo alilazimika kusitisha kwa mda kesi baada ya washtakiwa kuimba huku bwana Mosri akikataa kuvaa vazi la mahakamani akidai kuwa yeye nidye rais halali.
Mohammed Morsi alifikishwa katika chuo hicho kwa ndege aina ya helikopta kutoka eneo la siri ikiwa ndio mara yake ya kwanza kuwahi kuonekana hadharani tangu aondolewe mamlakani mwezi Julai mwaka huu.
Makundi ya waandamanaji tayari yamekusanyika nje ya chuo hicho cha mafunzo ya polisi huku wengine wakiimba nyimbo za kupinga jeshi la taifa hilo.
Maafisa wa kijeshi katika taifa hilo wanaendelea kushika doria katika mji wa Cairo na miji mingine baada ya wafuasi wa Bwana Morsi kuitisha maandamano makubwa.
Morsi aliondolewa uongozini kwa nguvu za jeshi mwezi Julai baada ya maandamano ya kila mara kufanyika kupinga utawala wake.
Ingawa alishinda urais kwa njia ya demokrasia, wakati wa uongozi wake wa zaidi ya mwaka mmoja, Morsi hakuelewana sana na taasisi nyingi za serikali.
Polisi na jeshi wamedhibiti hali ya usalama kote Misri
Baada ya kupinduliwa na jeshi, maandamano yalifanyika kila kulipokucha mjini Cairo na makubwa zaidi yalikuwa ya wafuasi wake kukesha karibu na kasri la rais wakitaka Morsi aachiliwe.
Polisi walaisababisha mamia ya vifo vya wafuasi hao walipovunja maandamano yao kwa nguvu.
Serikali ya muda pia imekuwa ikiwasawa na kuwakamata wanachama wa Muslim Brotherhood, chama chake Morsi.
Serikali pia imeharamisha vyama vyote vya kisiasa huku ikiwakamata mamia ya viongozi wa mashirika hayo.
Wafuasi wake wanasema kuwa alipinduliwa na jeshi na sasa anakabiliwa na kesi ya kisiasa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yameituhumu maafisa wa usalama kwa kufanya kazi yao bila uwajibikaji.

MJUMBE WA TUME YA MABADILIKO YA AVAMIWA NA KUUMIZWA VIBAYA


 MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia siku ya jumapili amevamiwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk. Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi, Dk. Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam, saa nane usiku alimdhibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa ni kweli baba yake ambaye aliwahi kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura kwa upande wake hazikutosha na hatimaye aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye aliyeshinda na kutangazwa kuwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi sasa alivamiwa na kujeruhiwa na mapanga na watu wasiyojulikana.
Dk. Natujwa anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alisema kwanza alipokelewa katika eneo la Emergence na kisha saa kumi na moja asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwa ajili ya kuanza kupewa matibabu.

WAPINGA KUAHIRISHWA KESI YA KENYATTA

Waathirika wa kesi inayomkabili rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa kutaka kucheleweshwa kwa kesi dhidi ya Rais Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini The Hague, Uholanzi.
Baadhi ya viongozi wa Afrika wameandaa rasimu ya azimio la kuomba kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja kwa masilahi ya usalama wa taifa, kufuatia shambulio la kigaidi katika kituo cha kibiashara cha Westgate mjini Nairobi.
Lakini mwanasheria wa waathirika, Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya kupatikana haki kwa waathirika. Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka yanayomkabili dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.

M23 YAWATAKA WAFUASI KUSITISHA MAPAMBANO

Wanajeshi wa serikali katika Jmauhuri ya kidemokrasi ya Congo, wanashambulia ngome ya mwisho ya waasi wa M23 katika maeneo ya milimani ,msituni Mashariki mwa nchi.
Mamia ya wakimbizi wanatoroka vita karibu na mpaka wa Mashariki mwa Congo na kuingia nchini Uganda.
Viongozi wa kundi hilo la M23 walitoa wito kwa wapiganaji wao kusitisha vita na kuruhusu mazungumzo ya amani na serikali.
Kiongozi wa wapiganaji hao Mashariki mwa nchi ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita vyao na jeshi la serikali.
Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.
Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.
Mazungumzo ya amani yanafanywa mjini Kampala, Uganda.

MEYA AKILI KUBWIA "UNGA"ASEMA HANG'ATUKI N'GO

Meya wa jiji la Toronto nchini Canada, Rob Ford amekiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine lakini amesema hatajiuzulu nafasi yake hiyo ya uongozi kwa kuwa ameshaomba msamana na haya ni mawimbi tu yatapita.

Kwa miezi kadhaa Meya huyo alikuwa akipinga habari ziliripotiwa kuhusu tuhuma za yeye kubwia dawa za kulevya, taarifa ambazo zilionekana kufifia nguvu na pengine kufa hadi siku ya Alhamisi ya wiki hii, pale Chifu wa Polisi wa Toronto, Bill Blair aliposema kuwa walikuwa wakifanya uchunguzi ambao asa umewawezesha kupata video isiyo na tashwishi ikimwonesha na
kuthibitisha kwa picha kuwa Ford ndiye mhusika aliyetajwa kwenye ripoti hizo na matukio ya kwenye video hiyo yanalandana na ripoti zilizotolewa kwenye mitandao mbalimbali.

Wakili wa Ford anapinga kwa kusema kuwa video husika haimwoneshi mteja wake akibwia unga.

Jumapili, katika kipindi cha redio kwenye kituo cha 1010 ambacho kinaendeshwa na Ford na kaka yake, Ford amemwambia Chifu wa Polisi airuhusu video hiyo ionekane kwa umma kwa kuwa wakazi wa Toronto wana haki ya kuiona na kuhukumu.

Video hiyo iliripotiwa kwanza na gazeti la Star na tovuti ya Gawker ambao wao walisema walioneshwa tu video hiyo katka nyakati tofauti na mtu aliyetaka kuwauzia ili waitumie kwa ajili ya habari, hivyo Gawker wakakusanya fedha na kuinunua na baadaye wakasema hawawezi kumtambulisha mtu aliyewauzia video hiyo kwa kuwa hawana mawasiliano naye tena.

Chifu wa Polisi, Blair yeye alisema waliipata video hiyo wakati wakichimbua kifa cha kompyuta, yaani 'hard drive' iliyokuwa imefutwa ili kuficha ushahidi wa dawa za kulevya.

Ford mwenyewe hakuzungumzia kuhusu kilichomo kwenye video hiyo akidai kuwa ilikuwa inahusika na uthibitisho wa madai ya tukio jingine ambalo kesi yake ipo mahakamani.

Ford ameomba msamaha kwa makosa ambayo hakuyaweka wazi. Alisema, “Mimi ni wa kwanza kukiri, rafiki, mimi ni wa kwanza kukiri, kuwa si mkamilifu. Nimekosa… na ninaloweza kufanya sasa ni kuomba msamaha kwa kukosea,” Ford amekaririwa na Reuters akitamka maneno hayo redioni na takriban saa moja baadaye akaongeza, “Nimekosea. Sijui nianzia wapi? Kwa mfano pale Danforth, ule ulikuwa ujinga kabisa. Sikupaswa kuwa-nzwiii pale Danforth. Kama umepanga kwenda kunywa chupa kadhaa za pombe, unapaswa kukaa nyumbani, basi. Huendi mbele ya kadamnasi na kujifanya shujaa mbele ya hadhara. Ninaomba msamaha kwa dhati kabisa, kwanza kwa familia yangu, pili kwa raia na tatu kwa walipa kodi wa jiji hili kubwa. Hakika siwezi kubadili yaliyopita, kilichobakia ni kusonga mbele na kujifunza kutokana na makosa na ninakuhakikishieni nimejifunza”

Reuters inasema, ikiwa unadhani kuwa sakata hili limeongoa imani ya wapiga kura kwa Ford, utakuwa umekosea kwani kituo cha CBC kimeripoti kuwa matokeo ya kura za haraka haraka yanaonesha kukubalika kwa Ford kumeongezeka kwa asilimia 5 na kufikia 44%.

Ijumaa, 11 Oktoba 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 10.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA KIWIRA STENDI YA MAGARI WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA.  MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA ISMAIL S/O
?,
MIAKA 25, KYUSA, MKAZI WA UYOLE,  ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE, FIMBO NA MARUNGU KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO. 

CHANZO NI TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MATUKIO YA UPORAJI WA PIKIPIKI NA KUWAUWA WAENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA –TUKUYU. 

MSAKO MKALI DHIDI YA WAUAJI UNAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAO WAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE. 
PIA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WALIKO WAHUSIKA WA TUKIO HILO WAZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.
 MNAMO TAREHE 10.10.2013 MAJIRA YA SAA  14:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KININGA KIJIJI CHA KAPALALA WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA THOMAS S/O GERVAS, MIAKA 42,MKIMBU,MKULIMA,MKAZI WA KIJIJI CHA KAPALALA AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA  GOBOLE BILA KIBALI. MBINU NI KUFICHA SILAHA HIYO KATIKA KIBANDA CHAKE KILICHOPO SHAMBANI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA BILA KUFUATA TARATIBU KWANI NI KOSA LA JINAI.  
Signed by:
 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Jumatatu, 29 Julai 2013

IDD AZZAN AZUNGUMZIA TUHUMA ZA KUFANYA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA

Siku chache baada ya jina lake kutajwa kwenye waraka unaodaiwa kuwa barua kutoka kwa mmoja wa Watanzania waliofungwa katika jela huko Hong Kong, Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan amezungumza na kusema kuwa yupo tayari kujiuzulu ubunge ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya.

Idd Azzan amekaririwa na chombo cha habari (via) jana akisema kuwa hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla. Akasema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake amedhamiria kumshushia heshima na huenda ana jambo limejificha.

Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.



Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwa nini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo?
Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani 


katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.

Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernard na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.

Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu.

Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni.

Alipoulizwa kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, Azzan alisema: “Ni ngumu kusema hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua.” 
Facebook Blogger Plugin by 2jiachie | 2jiachi